Msisubiri serikali kuu" - Waziri Mkuu

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, amezitaka Halmashauri nchini kutumia fedha za makusanyo ya ndani katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo badala ya kusubiri fedha kutoka serikali kuu pekee.

Amesema hayo leo Novemba 27, 2022, wakati alipokagua maendeleo ya ujenzi wa vyumba vya madarasa sita katika shule ya Sekondari ya Mwandege iliyopo Wilaya ya Mkuranga, Pwani.

Waziri Majaliwa amemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mkuranga Mwantumu Mgonja, kutenga kiasi cha shilingi milioni 120 kutoka kwenye mapato ya ndani kwa ajili ya kuanza ujenzi wa jengo la utawala katika shule hiyo ifikapo Januari 2023.

"Huu ni wakati wa kufanya kazi, nimeridhika na viwango vya ujenzi wa vyumba madarasa katika shule hii, endeleeni kusimamia viwango kwenye miradi mingine, twende na matakwa ya Rais wetu na kumsadia kutimiza maono yake ya kuwahudumia Watanzania", amesema Waziri Mkuu

Waziri Mkuu amesema kuwa mipango ya Rais Samia ni kuhakikisha kwamba serikali inawafikia Watanzania popote walipo hadi vitongojini kwa kupeleka huduma mbalimbali za kijamii ikiwemo afya, maji, shule, umeme pamoja na mawasiliano.

Mheshimiwa Majaliwa ametoa wito kwa wakulima wote nchini kutumia mvua hizi za mwanzo kuanza kujishughulisha na shughuli za kulima.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo