Rais Samia amepewa Ng'ombe 12

Mkoa wa Manyara umejenga madarasa 615 ya shule ya msingi na sekondari baada ya kupokea fedha kiasi cha Sh 21.4 bilioni katika mwaka 2020/22 kusaidia sekta ya elimu.


 Mkuu wa mkoa Manyara (RC), Makongoro Nyerere ametoa taarifa hiyo leo Novemba 23, 2022 katika uwanja wa Kwaraa Mjini Babati katika mkutano wa hadhara wa Rais Samia Suluhu Hassan.

Amesema katika mwaka huo wa fedha, Serikali imetoka Sh 37.5 bilioni kusaidia ujenzi wa barabara huku kiasi cha Sh 23.4 bilioni zilitolewa kukabiliana na tatizo la maji mkoa Manyara.

"Mheshimiwa Rais tunakushukuru sana kwani umetoa kiasi cha sh 10.2 bilioni kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu katika sekta ya afya lakini pia umetoa Sh 2.7 bilioni kusaidia miundombinu ya hifadhi za Taifa za Tarangire na Manyara," amesema

Makongoro Nyerere pia Serikali imetoka kisi cha Sh 5 billion katika soko la Madini Mererani, wilaya ya Simanjiro.

Katika mkutano huo, halmashauri saba za mkoa Manyara zilimpa zawadi mbalimbali Rais Samia Suluhu ikiwemo ng'ombe 12, mchele, vitunguu mwaumu na mavazi ya asili.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo