Wananchi waomba waruhusiwe kumuua Mama anayetuhumiwa kuua watoto wake


Watoto wawili wenye umri wa miaka kati ya miwili hadi mitano kutoka katika familia moja wameuawa kwa kucharangwa mapanga sehemu mbalimbali za miili yao na mtu anayedaiwa kuwa ni mama yao mzazi,

Jeshi la Polisi mkoani Mbeya tayari limeanza uchunguzi juu ya tukio hilo


Shan Yohana mama wa watoto hao ndiye anadaiwa kuwaua watoto wake kwenye nyumba wanayoishi, mashuhuda wa tukio hilo wamezungumza.


Akizungumza eneo la tukio, Mkuu wa Oparesheni Mkoa wa Mbeya, Abdi Issango amesema limetokea majira ya saa mbili asubuhi ambapo mazingira ya kifo hicho yanadhaniwa kuwepo kwa mgogoro  baina na mama  wa marehemu hao na familia  yake.


Tayari Jeshi la Polisi limewatia nguvu mama wa marehemu hao Shan Yohana, mdogo wake pamoja na mtoto aliyesalimika kwenye tukio kwa ajili ya hatua za kisheria na matitabu kwa majeruhi


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo