Precision Air kuwalipa fidia wahanga wa ajali

Shirika la ndege la Precision Air kupitia kwa mkurugenzi wake Patrick Mwanri limesema hawajaongea ama kutoa taarifa zozote kwa muda kutokana na sheria za anga kwani kuna taratibu zake mpaka pale uchunguzi utakapokamilika na wizara ndio inahusika na mamlaka husika kutoa taarifa za uchunguzi


Mkurugenzi huyo ametoa taarifa hiyo akiwataka wananchi kuendelea na utulivu mpaka uchunguzi utakapo kamilika akibainisha kuwa kila tukio linapotokea linaacha somo kwa wadau katika sekta akiwataka watu kuendelea kupata taarifa sahihi kutoka vyanzo sahihi.


Kuhusu suala la fidia kwa wahanga amesema shirika liko na bima na tayari taratibu za mawasiliano na wahanaga zinaendelea kuwajuza nini kinatakiwa ilikupata stahiki zao ikihusisha jumuiya ya kimataifa na inafanyika kwa faragha baina ya muhanga na kampuni


Hata hivyo ametumia fursa hiyo kuwashukuru watanzania serikali kuanzia kwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa namna walivyolipokea na kulishughulikia suala la ajali Na watahakikisha kila kitu kinaenda kwa utaratibu.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo