Maafisa wa polisi wa Kaunti ya Migori wametia mbaroni mwanamume aliyekuwa akijidai kwamba ni mwanamke, na kwa sasa wanaendela kumhoji.
Tukio hilo lilifanyika siku ya Jumatatu, baada ya maafisa wa Kituo cha Polisi cha Awendo Kenya, kumuona mtu aliyevalia mavzi ya kike ila mwili wake ulionekana kuwa ni mwanamume.
Katika ripoti ya polisi, maafisa hao walimuita mtu huyo na baada ya kumhoji walikuta ni mwanamume mwenye miaka 21 kwa jina Jared Opiyo Nyatumba, anayetoka Homa Bay na wala sio Sheila Bichange kama alivyodai.
Nyatumba aliwaambia polisi hao kuwa yeye huvaa ngu za wanawake kwa kuwa, ana urembomaumbile ya kike tangu utotoni.
"Alidai kwamba amekuwa na tabia za kike tangu utotoni ndipo akaamua kuvaa kama mwanamke," ripoti hiyo ilisema. Nyatumba alivalia rinda lizuri, ila polisi walikuta anakaa kama mwanamume na kumuamuru kuvua nguo hizo. Mara tu baada ya wenyeji wa Awendo kupata habari kwamba mwanamume aliyejidai kuwa mwanamke amekamatwa na polisi, walifululiza kwenye kituo hicho na kutaka wamuone.
Imeibuka kwamba mshukiwa huyo amehusishwa na visa vya mauaji kadhaa, yanayotekelezwa na mtu anayejifanya kuwa mwanamke na kutaka kumfunza adabu. "Wenyeji walipata kumuona mshukiw ahuyo kupitia dirisha la ofisi ya kutoa maelezo, ila wakasisitiza aachiliwe ili wampige kitutu," ripoti hiyo ilisema.
Chanzo: TUKO.co.ke
