Mchungaji atangaza kuwa anatafuta "Demu"

Mchungaji Kanyari amefichua kuwa yeye ni mwanamume mseja anayetafuta mwanamke wa kuoa. 


Akiongea na blogu moja humu nchini, Kanyari alisema kwamba hana haraka ya kuingia katika uhusiano lakini alikuwa na nia ya kuchumbiana na kipusa mrembo.


Kuhusiana na sura, mchungaji huyo mwenye utata alisema hana tatizo mradi apate kipusa atakayempenda na kumheshimu Miaka kadhaa baada ya mwimbaji wa nyimbo za Injili Betty Bayo na mchungaji huyo mwenye utata kutengana, alisonga na maisha na kupata mwanamume mwingine ila pasta huyo hadi sasa hajatapa mchumba. 


"Mimi bado sijaoa sana. Sijapata mtu. Nitafurahi ikiwa... nitapata msichana mzuri wa kuoa,..kuna wanawake wazuri hapa nje lakini sijaamua ni yupi bado," alisema. 


Kuhusu kushirikiana katik kuwalea wanawe na mama yao, mchungahi huyo alisema yeye hujukumikia maswala yao ya karo ya shule. "Watoto wangu wanaendelea vizuri na bado nawajukumikia. Nawalipia ada ya shule. 


Kushirikiana katika malezi ya watoto hata wakati mumetengana na penzi ni sawa, kila mmoja wetu anaelewa jukumu lake katika maisha ya watoto wetu," alisema. Aliwashauri wazazi kujukumika kikamlifu kuwalea watoto wao kwa ushirikiano hata kama wametengana. "Ni vizuri kuwalea watoto uliowazaa kwani hujui kama hao utakaowapata baada ya hapo watakuwa wako au hata watakupenda au kukuchukia. 


Ukiwa na uwezo wasaidie hata wengine kadhaa." Mapema mwaka huu, Kanyari alitamba mitandaoni baada ya kumuombea aliyekuwa mwigizaji wa Tahidi High, Omosh Kizangila, ambaye alionekana kuzidiwa na Roho Mtakatifu. "Nitakuombea ili nyota yako irudi. 


Ninakupa chakula kisha kukubariki kwa KSh 7,000.” Kisura ambaye alionekana kuwa asha wa kanisani, alijitokeza na kuelekea madhabahuni akionekana kubeba mfuko uliojaa vyakula kisha kampa Omosh ambaye nusra amwage machozi.

Chanzo: TUKO.co.ke 


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo