Wananchi waliovamiwa na kundi la vijana Wahalifu wenye silaha mbalimbali maarufu panya road huko Kibaha Mkoani Pwani wamesema vibaka hao waliwavamia kwa makundi huku wakisema hiyo ndio njia yao ya kupata rizki hivyo kila mtu atii amri ya kutoa anachoelekezwa
Wakizungumza kwenye makazi yao baadhi ya wahanga na majeruhi wa tukio hilo wanaeleza namna wezi hao walivyowavamia
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Pius Lutumo amethibitisha tukio hilo huku Daktari wa kitengo cha dharura katika hospitali ya rufaa ya Mkoa Tumbi. Dkt Oscar Feruzi akitaja idadi ya majeruhi waliotibiwa hospitalini hapo.
