Mtuhumiwa wa ujambazi Hoi baada ya Kuwagiwa maji ya moto

Mtuhumiwa wa ujambazi anauguza majeraha mabaya hospitalini baada ya jaribio lake la kupora kwenye nyumba moja katika kijiji cha Tuuti, Kaunti ya Bungoma huko Kenya kugeuka na kumletea balaa.


Kulingana na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Jinai (DCI), mwanamume huyo aliyekosa kutambulika alipenyeza nyumbani kwa Zipporah Masika, aliyekuwa akijiandaa kuoga majira ya asubuhi.


Zipporah alikuwa akienda bafuni akiwa amebeba maji moto ndipo akakutana na mwizi huyo, aliyekuwa ameiba simu yake na mali nyingine baada ya kuvunja nyumba. 


Ndipo mwizi huyo alipomsukuma, Zipporah alimchoma na maji ya moto usoni na kutoroka akiwa anapiga kamsa na kuwashutua majirani waliofika katika boma hilo.


Hata ingawa mwizi huyo alikuwa na majeraha usoni ya kuchomwa, wanakijiji walianza kumpiga kitutu na hata ingawa aliwalilia wamuonee huruma, hakusikizwa na kuzidi kuongezwa majeraha. Wakati polisi walipofika pale, mwizi huyo alikuwa anatirikwa na damu kwa kukatwa kichwani na wanakijiji ambao walionekana kutaka kummaliza. 


Maafisa hao walimkimbiza mwizi huyo katika Hospitali ya Rufaa ya Kaunti ya Bungoma, ambako kwa sasa yuko hali mahututi akijaribu kupigania uhai wake.

Chanzo: TUKO.co.ke 


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo