Kioja kilishuhudiwa katika Mahakama ya Embu nchini Kenya siku ya Jumatatu, Novemba 7, 2022 wakati mwanamume anayeshtakiwa kwa wizi alipatikana na mkoba wa wakili wake.
Akisimulia kisa hicho, wakili Faith Japann wa mahakama kuu, alisema alikuwa amefika kortini kumwakilisha mshtakiwa wakati mwendeshaji mashtaka aliwasilisha mkoba wake uliopotea miongoni mwa vitu ambavyo mteja wake alipatikana navyo.
Ilikuwa ni wakati wa upande wa mashtaka kuwasilisha kesi ambapo alitambua mkoba wake ambao kwenye hafla ya umma. "Nilikuwa nikimshikilia mwenzangu na nilishangaa nilipogundua kuwa mshtakiwa alikuwa na mkoba wangu," Jappann alisema.

Hata hivyo, mshtakiwa alikana mashtaka hayo. Kesi hiyo itatajwa Jumatatu, Novemba 28, huko Embu. Wakili huyo alikuwa bado hajaamua kama atamshtaki mwanamume huyo kwa madai ya kuiba mkoba wake au kuendelea kumwakilisha.
Chanzo: TUKO.co.ke