Mchungaji Aeleza anavyoelemewa na Idadi Kubwa ya Wanawake Wanaomtongoza

Mhubiri tatanishi Victor Kanyari ni mwanamume mseja anayehangaishwa na idadi kuwa ya wanawake wanamtongoza hususan kwenye mitandao ya kijamii.


Katika mahojiano na Nairobi News, Kanyari alisema kuwa wanawake wamefurika katika DM zake kiasi cha kwamba wengine wanamtumia picha zao za uchi.


Licha ya wanawake wengi wanaomtongoza kuwa wa mitandaoni, mhubiri huyo anasisitiza kuwa hawezi kumchagua mwanamke kwa mitandao ya kijamii. "Wanawake wananitongoza mitandaoni, wananitumia picha chwara na mazagazaga yote. Sitaki kuahidi kuwa nitawajibu. Siwezi kumchagua hivyo tu mwanamke kutoka kwa mitandao ya kijamii," Kanyari alisema.


Mnamo Oktoba 16, 2022, TUKO.co.ke iliripoti kuwa Pasta Kanyari alikuwa na mpango wa kutafuta mwanamke wa kuoa miaka kadhaa baada ya ndoa yake kusambaratika. 


Mhubiri huyo tatanishi alisema kuwa hana tatizo na sura ya mwanamke huyo anachotaka ni kupata kipusa atakayempenda na kumheshimu. "Mimi bado sijaoa sana. Sijapata mtu. Nitafurahi ikiwa nitapata msichana mzuri wa kuoa. Kuna wanawake wazuri hapa nje lakini sijaamua ni yupi bado," Kanyari alisema. 

Chanzo: TUKO.co.ke 


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo