Makete; Mtoto auawa Kinyama, Mtuhumiwa asema "Alinitukana"

Matukio ya Ukatili yameendelea kujitokeza katika maeneo mbalimbali ambapo katika Wilaya ya Makete mkoa wa Njombe mtoto Atu Sanga (4) aliyekuwa mkazi wa Kijiji Cha Utweve wilayani hapo, amekutwa ameuawa kinyama 


Mtoto huyo alipotea usiku wa kuamkia Novemba 1, 2022 kabla ya kukutwa akiwa amefariki dunia hali iliyoleta taharuki katika kijiji husika kutokana na kudhani kuna matukio ya mauaji ya watoto yanaendelea


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe Hamis Issah amesema "Jeshi la polisi tulitulia na kuanza upelelezi wa kina na tunajua asili ya matukio ya mauaji ya huko, tulifanya uchunguzi na matokeo yake katika familia zile kukaonekana kuna kijana mmoja hayupo"


Amesema juhudi zilifanyika na kijana huyo alitafutwa na alipatikana na baada ya kuona kundi la watu wengi alitimua mbio, lakini amekamatwa


Amemtaja kijana huyo kwa jina la Joshua Justin Asheri Sanga ambaye ni mwanafamilia na alipohojiwa alikiri kuhusika na mauaji hayo ambapo amesema "Tunasikitika kidogo, tukio limetokea na mtoto mdogo amepoteza maisha lakini kijana huyu taarifa zake zilikuwa hazijulikani kuwa ndio yeye muhusika lakini amekiri yeye mwenyewe hata fimbo yake aliyompigia huyo mtoto ameionyesha"


Kamanda Issa amesema mtoto huyo  amevunjwa mabega yote mawili kwani inaonesha fimbo hiyo ilipiga kwenye mabega na kichwani kuna mbonyeo mkubwa ambapo baada ya kukiri kufanya kitendo hicho amesema sababu zilizomfanya akimbie ni kutokana na kuona askari wakiwa wamebeba bunduki


"Na kitendo kingine alichokisema ni kwa nini amefanya hivyo amedai mtoto huyu alimtukana, jamani jaribuni kufikiria mtoto wa miaka 4  amemtukana mtu mkubwa huyu kijana ana umri zaidi ya miaka 18 na kutoa adhabu ambayo ni kubwa kiasi hicho, jamani Njombe tusiwe kama sikio la kufa halisikii dawa, sisi tunasema hivii jeshi la polisi hatuwezi kuwa watu wa aina hiyo" amesema kamanda Issa

TAZAMA VIDEO HAPA CHINI UPATE UNDANI WA TUKIO HILO





 


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo