Jela miaka 30 kwa kuwa na Uhusiano wa Kimapenzi na mwanafunzi

MAHAKAMA ya Wilaya ya Iringa imemuhukumu kifungo cha miaka 30 Baraka Mwinuka (30) kwa kosa la kuwa na mahusiano na Mwanafunzi mwenye umri wa miaka 11 aliyekuwa akisoma darasa la 6 katika Shule ya Msingi Ngome iliyopo Manispaa ya Iringa.


Baraka alikuwa akiishi jirani na nyumba ya Mwanafunzi huyo na alizijua ratiba zote za Wazazi wa Mwanafunzi kwamba Mama anafanya kazi dukani na Baba dereva bajaji na mwanafunzi huyo alikuwa akirudi kutoka masomoni saa nane mchana.


Kwa mujibu wa Mahakama siku ya tukio mtuhumiwa alibeba chips mayai na soda na alifanya tukio hilo chumbani kwa mwanafunzi huyo, baada ya kurudi nyumbani mama alikuta mashuka ya kitanda cha mwanafunzi yamebadilishwa na alipomuhoji kwa ukali binti akamwambia Baraka alikuja na kumuingilia.


Kesi hiyo imesimamiwa na Mwendesha mashtaka wa Serikali Magreth Mahundi na ameiomba Mahakama kutoa adhabu kali ili iwe fundisho kwasababu vitendo vya ukatili kwa watoto vimeendelea kushamiri.


Hata hivyo Mahakama ilipompa nafasi ya kujitetea mtuhumiwa aliendelea kukataa kuwa hajafanya tukio hilo ndipo Mahakama ikamuhukumu kifungo cha miaka 30 kwa kosa la kuwa na mahusiano na mwanafunzi mwenye umri wa miaka 11.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo