Nauli za Mabasi na Stendi ya Tandala vyarudishwa kwenye kamati ya Fedha

Suala la Matumizi ya stendi ya Mabasi Tandala pamoja na nauli ya mabasi kutoka Njombe hadi Makete limeibua mjadala kwenye baraza la madiwani wakati wa uwasilishaji wa taarifa za kamati ya fedha, mipango  na utawala

 

Akichangia hoja za kamati hiyo Novemba 02, 2022 Diwani wa kata ya Kipagalo Nehemia Sanga amezungumzia suala la nauli kuwa juu licha ya ujenzi wa barabara ya Makete Njombe kwa kiwango cha lami na LATRA kutoa bei elekezi lakini pia akizungumzia kusuasua kwa matumizi ya stendi ya mabasi Tandala


Kuhusu suala la Stendi ya Mabasi Tandala diwani huyo amesema maagizo waliyoyatoa kuwa itumike yanatakiwa kusimamiwa ili manufaa ya pande zote yaani wananchi na serikali yaonekane


Hawa Kader ni Kaimu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete amesema suala la stendi ya mabasi Tandala maamuzi yalishafanyika na kuzua mjadala kwenye mitandao hivyo inapotokea maamuzi yamefanyika na utekelezaji wake kushindwa kusimamiwa inasababisha kero hivyo wao kama viongozi wanatakiwa kutoa majibu na sio kuwa wachochezi


Kwa Upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Makete William Makufwe amesema suala la nauli ni kweli hazitozwi kwa viwango vilivyotolewa na LATRA hivyo suala hilo ameombwa lipelekwe kwenye Kamati ya Fedha ya Halmashauri hiyo na watamualika Meneja wa LATRA mkoa aweze kushiriki ili watoke na maamuzi baada ya majadiliano

Kuhusu suala la Stendi ya Mabasi Tandala Mkurugenzi Makufwe amesema wamejitokeza watu kupinga matumizi ya stendi hiyo kwa kusema matumizi yake yanatesa watu suala ambalo amesema haliko sahihi sana kwa kuwa si kweli kwamba kila abiria anayekwenda Ikonda ni kwa ajili ya matibabu au ugonjwa


Amesema kwa sasa kumekuwa na stendi tatu katika mji mmoja yaani ya Tandala, ya Njia panda ya Hopsitali na ile ya Hospitali ya Ikonda hivyo suala hilo ashauri nalo lirudishwe kwenye Kamati ya Fedha, Mipango na Utawala kwa ajili ya kulijadili kwa maslahi mapana ya wananchi huku akisisitiza wakati mwingine watu wasiogope kubeba lawama kwenye mambo ya maendeleo kama hayo.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo