Ahmed Ally alivaa sakata la Kibu Denis


Meneja wa Habari na Mawasilino wa Simba SC Ahmed Ally amejitokeza hadharani na kumkingia kifua Kiungo Mshambuliaji wa Klabu hiyo Kibu Denis.


Kiungo huyo amekuwa na wakati mgumu msimu huu, huku akionyesha kushindwa kuwajibika kwa kuifungia Simba SC mabao muhimu licha ya nafasi anazopata kila anapopewa nafasi na Kaimu Kocha Mkuu Juma Ramadhan Mgunda.


Ahmed Ally amechukua jukumu hilo, kwa kuandika ujumbe mzito kwenye kurasa zake za Mitandao ya Kijamii kuhusu Kibu, ambaye alisajiliwa Klabuni hapo mwanzoni mwa msimu uliopita akitokea Mbeya City FC.


Ahmed Ally ameandika: Kila mmoja hupitia nyakati ngumu kazini.

Kibu Denis anapitia nyakati hizo, jukumu letu ni kusimama nae na kumtia moyo ili isimuathiri
Kwenye football ukipatia utapatia tena, na ukikosea unaweza kukosea tena ni jukumu letu kumpa support ili asikosee tena.

Hatupaswi kumpa presha tunapaswa kumpa imani kwamba anaweza kufanya makubwa kama alivyofanya msimu uliopita🙏


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo