Abiria 26 kati ya abiria 43 wameokolewa

Ndege ya Precision Air iliyopata ajali wakati wa kutua Bukoba leo ilikuwa imebeba abiria 43 ambapo hadi sasa wameokolewa 26 tu na kupelekwa hospital ya Rufaa ya mkoa Kagera.


Akitoa taarifa ya idadi hiyo Mkoa wa Kagera Albert Chalamila amewaomba wananchi kuendelea kuwa watulivu maana mawasiliano na marubani walioko ndani ya ndege bado yanaendelea.


Ndege hiyo ni ATR 42 yenye namba za usajili 5H BWF ambayo ilikua ikitokea Dar es salaam kuelekea Bukoba na ilikua na safari ya kurudi Dar es salaam kupitia Mwanza.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo