Tanzania Prisons na Singida Big Stars zafungiwa kusajili Ligi Kuu

Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imezifungia kusajili klabu za Ligi Kuu ya NBC za Tanzania Prisons na Singida Big Stars kwa kosa la kusajili wachezaji wenye mikataba na klabu zingine.


Uamuzi wa Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji umefanywa kwa kuzingatia Kanuni ya 47(21) ya Ligi Kuu baada ya kuzikuta na kosa hilo. Adhabu hiyo ni kwa dirisha moja la usajili.

Tanzania Prisons ilimsajili kipa Musa Mbise wa Coastal Union wakati ikifahamu kuwa bado ana mkataba na klabu hiyo. Nayo Singida Big Stars ilimsainisha mkataba kipa Metacha Mnata huku akiwa bado ana mkataba na klabu ya Polisi Tanzania.

Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji imezikumbusha klabu zote nchini kuwa usajili wa wachezaji unafanywa kwa kuzingatia kanuni, na ambazo zitakiuka kanuni zitachukuliwa hatua kwa mujibu wa kanuni.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright 2025 EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo