Ikiwa zimepita siku chache tangu kuonekana kipande cha video kikimuonesha Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania Dkt Tulia Ackson akiwataka watanzania kutokumzungumzia vibaya Mh Rais Samia Suluhu Hassan, jana Dkt Tulia ametolea ufafanuzi juu ya kipande hicho kilicho sambaa mitandaoni.
Akizungumza mara baada ya kufungua kongamano la wanawake wachungaji wa kanisa la Moravian Tanzania uliofanyika Jijini Mbeya, amesema aliyesambaza kipande hicho alikua na nia ovu dhidi yake na kwamba hashangazwi na hatua hiyo kwakua ni hali ya kawaida katika siasa.
Dkt Tulia amesema kipande kichokamilika kipo ikiwa mtu anapenda kupata taarifa kamili anaweza kufuatilia badala ya kusabaza habari za uongo kwa kukatwa vipande vinavyoleta taharuki na kusambaza.