Kufuatia vifo saba vya familia moja akiweko Ofisa wa uhamiaji wa uwanja wa ndege wa kimataifa KIA Serikali imeonya jamii na familia husika kwamba hauna mkono wa mtu katika ajali hiyo.
Akiongoza mamia ya waoombolezaji Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Nurdin Babu amesema nyakati kama hizi jamaii huingiwa na imani potofu Kutokana na uzito wa tukio husika.
Babu amesema huu ni wakati wa familia na jamii kwa ujumla kuwafariji wafiwa huku wakijawa na imani ya Mungu matukio hayo hutokea ni mipango ya Mungu.
Akiongoza misa ya kuaga Miili hiyo Padri wa Parokia ya Hai Jimbo Katoliki Moshi Faustine Furaha ameitaka jamii kujiandaa na maisha ya hapa duniani.
Naye mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM Mkoa wa Kilimanjaro Patrick Boisafi amewataka watumiaji wa vyombo vya moto kuheshimu na kutii alama za usalama barabarani.
Amesema pamoja na kwamba huu sio wakati wa kulaumiana bali ni vyema watumiaji wa vyombo hivyo kutii sheria hizo za usalama barabarani ambazo zitaepusha ajali zisizo za lazima.
Tukio la kuiaga miili hiyo saba limeafanyika katika mtaa wa Kingereka , Kata ya Muungano Wilaya ya Hai na kuhudhuriwa na viongozi wa Serikali, dini, siasa ,na kamati ya usalama ya Mkoa.
Na Martha Fatael, TimesMajira Online, Hai.