Jeshi la polisi mkoa wa Simiyu linamshikilia mzee mmoja mwenye umri wa miaka 65, mkazi wa kijiji cha Mpindo wilayani Maswa mkoani Simiyu, kwa tuhuma za kumbaka mtoto mwenye miaka mitano ambaye ni mjukuu wake.
Kamanda wa polisi mkoa wa Simiyu ACP Blasius Chatanda amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema limetokea Oktoba 09 mwaka huu 2022 majira ya saa 10 jioni.
Amesema mtuhumiwa huyo aliyetambulika kwa jina la Mahona Mboje alitenda tukio hilo wakati bibi wa mtoto huyo akiwa ameenda kuchunga mifugo na kueleza kiini cha tukio hilo kuwa ni tamaa ya mapenzi.
Mtuhumiwa amekamatwa na yupo mahabusu kwa mahojiano na anatarajiwa kufikishwa mahakamani.
Kamanda wa polisi mkoa wa Simiyu anatoa wito kwa wananchi kuacha tabia ya kujihusisha kimapenzi na watoto kwani jeshi la polisi halitasita kuwachukulia hatua kali ikiwemo kifungo cha miaka 30 jela au kifungo cha maisha.