Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Dar es Salaam kimelaani vikali kitendo cha watu kuvamia na kuvunja ofisi ya Chama hicho Kata ya Kinondoni Oktoba 10, 2022.
Akizungumza kuhusu tukio hilo, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Kate Kamba, amesema watu hao wanadai kumiliki eneo hilo kihalali huku akieleza eneo ni eneo la CCM tangu mwaka 1971 na kuwa linanyaraka zote za umiliki ambazo ni halali kisheria.
Aidha, amesema hatua kali zitachukuliwa dhidi ya watu hao ambao tayari wamebainika, huku akitoa onyo kwa watu wote ambao wenye nia ya kuharibu, kuiba mali au nyaraka za chama kwa kutumia njia zozote, na kuwa watachukuliwa hatua kali za kisheria.