Rais Samia: Kuna ambayo ni mepesi tunaweza kuyafanyia kazi haraka

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, amepokea ripoti ya kikosi kazi kilichoundwa ili kutoa maoni na mapendekezo ya kufanyiwa kazi katika masuala mbalimbali ya demokrasia na siasa.

Baada ya kupokea taarifa hiyo, Rais wa Tanzania Samia suluhu Hassan amesema kuwa jambo la katiba ni la muda mrefu

 “Hili la Katiba mpya mtakwenda kulifanyia kazi na mtaleta mapendekezo yatakayotangazwa Watanzania wote wayaelewe, Mimi nakubaliana kuwa ni jambo la muda mrefu lakini muhimu Watanzania wote waelewe’’ amesema Samia

Rais Samia aliongeza kuwa mchakato wa katiba ni suala la pekee na lenye kazi nzito.

kwa upande mwingine kikosi kazi hicho kilitoa mapendekezo juu masuala mbalimbali ikiwemo kuruhusiwa kwa mikutano ya vyama vya siasa na ukomo wa wabunge wanawake wa viti maalum.

 “Utaratibu wa kuwa na viti maalum vya wabunge, wawakilishi na madiwani wanawake uendelee isipokuwa sheria ziboreshwe kuweka ukomo wa miaka 10 kwa mtu kuwa mbunge mwakilishi, alisema Prof. Mukandara.

Rais Samia aliongeza kuwa baada ya mapendekezo hayo, kuna masuala ambayo wanaweza kufanyia kazi kwa muda mfupi na mengine kwa muda mrefu.

“Kuna ambayo ni mepesi tunaweza kuyafanyia kazi haraka, lakini kuna yale ambayo lazima tukae na kuangalia sheria zilizopo zina mapungufu wapi? Na tunayabadilisha vipi kutokana na maoni yenu,” amesema Rais Samia. 


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright 2025 EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo