Rais Samia awapandisha madaraja watumishi 262,800

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora), Jenista Mhagama amesema Rais Samia Suluhu Hassan amewapandisha madaraja watumishi 262,800 hadi kufikia Septemba 2022.


Waziri Mhagama ametoa kauli hiyo mbele ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati alipopewa nafasi kuzungumza na viongozi wa mkoa, wilaya na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba mkoani Ruvuma kwenye kikao alichokiitisha ili kuwakumbusha watumishi wajibu wao

“Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan hadi kufikia Septemba, 2022 ameshawapandisha madaraja watumishi 262,800 ambao kwa miaka zaidi ya mitano walikuwa hawajapanda. Na kila mwezi Serikali inatumia sh. bilioni 58.3 kulipia mishahara iliyopandishwa”


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright 2025 EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo