Mtoto wa miaka 10 adaiwa kumuingilia kimwili mwenzake

Mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka 10 katika mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar (Jina linahifadhiwa)  anadaiwa kumuingilia mtoto wakike mwenye umri wa miaka 2 


Mama wa mtoto aliyefanyiwa kitendo hicho amedai kuwa aligundua tukio hilo wakati akimuogesha mtoto wake na alipomuuliza nani amefanya kitendo hicho alimtaja mtoto mwenzake kuwa anahusika

Jitihada za kumtafuta mama wa mtoto anayedaiwa kutenda kitendo hicho zimegonga mwamba baada ya kukataa kutoa ushirikiano 


Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Mjini Magharibi Richard Thadeo Mchomvu ameitaka jamii kuishi katika mila na desturi na kuwalea watoto katika misingi ya dini ili kuepuka matukio kama hayo


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright 2025 EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo