Wananchi wa eneo la Mnali, Manispaa ya Lindi, wameipongeza serikali kwa ujenzi wa jengo la kisasa maalumu kwa akina mama kujifungulia, ambapo hapo awali wananchi hao waliamua kujenga kibanda cha miti ili kiwasaidie kwani walikiri kuchoka kudhalilika kutokana na chumba wanachokitumia wakati wakati wa kujifungua kuwa kidogo na pia kutumika na wagonjwa wengine.
Baada ya taarifa ya adha waipatayo akinamama hawa kufika katika Ofisi ya Rais TAMISEMI na kutolewa majibu ya utekelezaji wa haraka kupitia mitandao ya kijamii, Manispaa ya Lindi imeanza kusimamia ujenzi huo na kwa hatua za awali wananchi hasa akina mama wamejitolea kuchimba msingi na kukusanya mawe.
Huku wanawake hao wakiiomba serikali ujenzi huo usikawie kwani bado adha ya kujifungua kwenye chumba wasichopendezwa nacho, inaendelea.