Wafariki dunia, Wengine wajeruhiwa ajalini Mbeya

Watu wawili wamefariki na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya basi la Kyela Express kugongana uso kwa uso na basi dogo aina ya Toyota Coaster lililokuwa likisafirisha msiba kutoka mkoani Dodoma kwenda wilayani ya Kyela.


Mkuu wa Wilaya ya Rungwe mkoani hapa, Dk Vicent Anney amethibitisha kutokea ajali hiyo alipozungumza kwa simu na Mwananchi Digital leo Jumanne Oktoba 11, akisema imetokea majira ya saa 2.30 za asubuhi katika kijiji cha Ibula Kata ya Kiwira.

“Ni kweli ajali hiyo imetokea leo na mpaka natoka eneo la tukio kuna vifo vya watu wawili lakini kwa upande wa majeruhi bado sina idadi kamili nafuatilia ntakupa taarifa kamili,” amesema Anney.


Kwa upande wake Diwani kata ya Kiwira Wilaya ya Rungwe, Michael Simon aliyezungumza pia kwa simu, amesema basi la Kyela Express lilipopofika eneo la Kanyegere iligongana na gari aina ya Costa na watu waliopoteza maisha na majeruhi walikuwa ndani ya Costa hiyo.


''Watu waliofariki papo hapo ni wawili na majeruhi ambao nimewashuhudia ni zaidi 15 walikuwa kwenye Coster iliyokuwa ikisafirisha msiba ambayo inaonyesha ilikuwa katika mwendo kasi na ililivaa basi la Kyela Express,” amesema.


Simon amesema kuwa wakati ajali hiyo ikitokea gari lililokuwa limebeba maiti lilikuwa limetangulia huku akieleza chanzo cha ajali ni mwendo kasi wa dereva wa Coaster aliyekuwa akisafirisha msiba kwenda Kyela.


Hata hivyo, ameshukuru huduma ya uokozi iliyofanywa na Jeshi la Polisi na Jeshi la Zimamoto chini ya usimamizi wa Mkuu wa Wilaya ya Rungwe, Dk Anney.


''Tunashukuru kwa Jeshi la Polisi na kikosi cha zimamoto kufika kwa wakati eneo la tukio na kufanya uokozi ikiwa ni pamoja na kukimbia Majeruhi hosptali,” amesema.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya hakupatiakana kuzungumzia ajali hiyo.


Chanzo:Mwananchi


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo