Kikosi kazi cha kuratibu maoni ya wadau kuhusu demokrasia ya vyama vingi nchini Tanzania, kimependekeza mikutano ya hadhara iruhusiwe sambamba na mabadiliko ya sheria mbalimbali zitakazowezesha mikutano hiyo kufanyika kwa ufanisi.
Hayo yamebainishwa leo Ijumaa, Oktoba 21, 2022 Ikulu jijini Dar es Salaam na mwenyekiti wa kikosi kazi, Profesa Rwekaza Mukandala wakati akiwasilisha mapendekezo ya kikosi hicho kwa Rais Samia Suluhu Hassan.
Amesema baada ya kikosi hicho kufanya kazi kwa miezi 10 kikichambua maoni mbalimbali ya wadau, kinapendekeza kwamba mikutano ya hadhara iliyozuiliwa mwaka 2016, iruhusiwe kufanyika.

Viongozi pamoja na Wajumbe wa Kikosi Kazi kuhusu Uratibu maoni ya wadau wa Demokrasia ya Vyama vingi vya Siasa wakisikiliza hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 21 Oktoba, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Mwenyekiti wa Kikosi Kazi kuhusu Uratibu maoni ya wadau wa Demokrasia ya Vyama vingi vya Siasa Profesa Rwekaza Mukandala, Makamu Mwenyekiti Hamad Rashid Mohamed pamoja na Wajumbe wa Kikosi Kazi hicho mara baada ya kupokea Ripoti yao Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 21 Oktoba, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Mwenyekiti wa Kikosi Kazi kuhusu Uratibu maoni ya wadau wa Demokrasia ya Vyama vingi vya Siasa Profesa Rwekaza Mukandala pamoja na Makamu Mwenyekiti wa Kikosi Kazi hicho Hamad Rashid Mohamed mara baada ya kupokea Ripoti ya Kikosi Kazi hicho Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 21 Oktoba, 2022. PICHA NA IKULU
JIUNGE NA EDMO BLOG SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube
Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi