Na Kenneth Ngelesi, Ludewa
KAMPUNI ya (NGMC) inayo jihusisha na masula ya utafiti wa Madini inayo milikiwa na Mzungu Alfred Novose raia wa Austria ya jiji Dar-es-salaamu inatuhumiwa kuvunja sheria za nchi kwa kuendesha vitendo vya utapeli kwa wachimbaji wadogo wa madini wilayani
Ludewa katika mkoa mpya wa Njombe Njombe.
Habari za kuaminika na Tanzanmi Daima ilizipata kutoka kwa wachimbaji wadogo kutoka wilayani na zinaeleza kuwa kampuni hiyo imesajioliwa kisheria lakini imekuwa haina ofisi kwa upande wa Dar-es-salaamu wala wilayani Ludewa.
Aidha habari kutoka kwa wachimbaji hao zinaeleza kuwa kampuni hiyo ilisajiliwa miaka minne iliyopita na Mwenyekiti wa bodi ni Mbunge wa zamani wa jimbo la Makete na Waziri aliowai kuwa waziri katika Serikari ya awamu ya tatu muhula wa pili wa uongozi wRaisi Mbenjamini Mkapa na Mkurugenzi wa zamani wa idara ya usalama wa Taifa, Hansi Kitine.
Wakizungumza na waandishi wa habari , miongoni mwa wachimbaji wadogo wanao daiwa kutapeliwa na kudhulumiwa na Raia huyo kutoka Austaria ni mmiliki wa kampuni ya wachimbaji wadogo ya Sarah and Partiners ,Sarah Lusambagula, ambaye amedai kutapeliwa viwanja 346 vya kuchimba madini ya shaba,pamoja na fedha milioni mbili.
Lusambagula alisema kuwa walifahmiana na mzun gu huyu mwezi Ausgust mwaka jana kupitia kwa Kitine baada ya kutambulishwa wakati wakihaha kutafuta mtu wa kuweza kafanya nae kazi za uchimbaji katika maeneo ambnyo walisha pewa Leseni ya jkundeshea shughuli za uchimbaji.
'Kwakuwa baada ya kufahamiana na na wakati huohuo tulikuwa na shida na kufafuta mtu wa kufanya naye kazi na imani tulikuwa nayo kwa watu qweupe kama mnavyo juu pia kwa kuwa alikuwa na Kitine na nafasina kwa heshim,a yake aliyo kuwa nayo tulimwamini na kuweza kumpa mchanga wa sampuli ya madini ya Kopa tani tatu ambazo ali ituma gari kuja kuchukua site' alisema Lusambagula.
Alisema kuwa sabbu ya kumpa sampli hiyo ilimkuwa kwenda kupima ni kujua kiasi cha madini hayo na hapo ni baada ya kukubaliana mambo mbalimbali kuhusu uchimbaji wa madini walimkabidhi kiasi hicho cha sampuli kwa lengo la kupima kiwango cha madini hayo ya Shaba kabla ya kazi ya uchimbaji kuanza.
Aliongeza kuwa tangu walipomkabidhi kifusi hicho cha sampulihawakuwa na mawasiliano mazuri kutokana Mzungu huyo kubadilika na kila akipigiwa simu alikuwa hapokei na walipomtafuta Kitine aliyewakutanisha naye hakuwapa uhakika.
Alisema cha kushangaza mapema mwezi huu , Mkurugenzi huyo Voseli raia wa Austria aliwapigia simu na kuwataka wakutane Jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuendeleza mazungumzo ya uwekezaji baina yao nao bila kusita waliitia wito huo.
“Tullipofika Dar es salaamu tulikutana chini ya Kitine namoja ya masharti yetu tulitaka kulipwa kwanza fedha ya sampuli alichukua kiasi cha shilingi milioni mbili, kwa kweli walitumia lugha laini wakitutaka tuwe na subira”
Aliongeza kuwa baada ya makubaliano hayo mzungu huyo aliomba na kuahidi kulipa deni hilo pindi tu atakapopofanikiwa kufika wilayani Ludewa kwa lengo la kuona eneo la uchimbaji, ambapo Aprili 13 walifika wilayani humo na kutambulishwa kwa Mkuu wa wilaya na siku iliyofuata walienda eneo la machimbo katika kijiji cha Ibumi.
Lusambagula aliendelea kueleza kuwa baada ya kufika katika eneo hilo la machimbo ambalo walikuwa wakilimiki walishangaa kuona mzungu huyo akianza kupima maeneo kwa kutumia mashine bila kuwashirikisha.
“Kwa kweli Teknolojia hizi ni hatari sana, jamaa alikuwa amekaa kwenye gari lakini sisi bila kujua , tulifikiri alikuwa akipiga picha za kawaida kumbe alikuwa anaiba kodineti zetu na isingekuwa wale wasamalia ali ongozana nao kutushtua sasa tungekuwa tunalia”.
Alisema baada ya kupata taarifa hizo walimbana na kubainikuwa tayari alikuwa amepima kilomita zaidi ya 30 na kuiba alama za mipaka ya eneo hilo (CODENETS) lenye viwanja 346, ambapo baada ya hapo angeweza kwenda Wizara ya Nishati na Madini kuvilipia na kumilikishwa.
'Baada ya kupata taarifa hizo hamuwezi amini niliamua kumvaa huyo mzungu na kukamatana mashati kwa lengo la kutaka anipe hizo CODENET kwa kweli alioachia baadhji ya ka karatasio ambaszo alisha chapa zinzo onyesha hizo namba na maeneo yaliyo na madini' ugomvi wenyewe ulitokea katioka Hotel ya Mkongoti namo Aprili 18 mwaka huu' alisema Luambagula
Hata hivyo taarifa zinadai kuwa tayari mzungu huyo alishachenjua kifusi hicho na kupata kiasi cha wakia 30 kutokana na madini ya aina tatu yaliyopatikana kutoka kwenye kifusi hicho cha sampuli na kuziuza kwa sh.milioni 12.
Dira ya Mtanzania ilimtafuta mzungu huyo alipoulizwa kama anafahamianana Sarah na amewahi kupokea sampuli ya madini hayo ya shaba, alikuwa mkali kwa kumwambia mwandishi wetu kuwa kiama angeandika habari hiyo ajiandae kwenda mahakamani.
Lakini alipobanwa zaidi alikiri kupokea kifusi cha sampuli hiyo tani tatu na kwamba baada ya kuzifikisha Jijini Dae es salaam alibaini kuwa ni takataka hivyo naye kugundua kutapeliwa hivyo kuamua kuwashitaki mahakamani, lakini bila kutaja ni mahakama gani alikofungua mashitaka.
Akizungmzia mkasa huyo baada ya kulizwa wa waandishi wa habari kwa njia ya simu Kitine, alikiri kuwa ni Mwenyekiti wa bodi nakueleza kuwa suala hilo halina umuhimu kuandikwa na vyombo vya habari kwa kuwa tayari pande zote mbili yaani Kampuni yake na Sara zilisha kutana na kuzumgum,zia suala hilo na utata ambao uliojitokeza.
Alipotakiwa kueleza tuhuma kuwa kampuni hiyo haina ofisiwala wafanyakazi alijibu kuwa hilo si suala la msingi kwa kuwa uamuzi wa mtukufungua ofisi au kuigeuza nyumba kuwa ofisi ni la kwake wala si la mtumwingine na.
Mwisho.
|
KAMPUNI YA MADINI YATUHUMIWA KUVUNJA SHERIA ZA NCHI HUKO LUDEWA
By
Unknown
at
Thursday, April 26, 2012