Miaka saba jela, faini ya milioni 15 kwa kumkashifu Rais Samia

Mwanaume afungwa miaka 7 kwa kumtukana raisMahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Simiyu imemhukumu kifungo cha miaka saba na faini ya Sh15 milioni, Levinus Kidanabi maarufu kama 'Chief Son's kwa makosa matatu ikiwamo kumkashifu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.

Hukumu hiyo imetolewa Oktoba 19, 2022 na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Matha Mahumbuga ambapo alieleza kuwa mtuhumiwa alitoa taarifa za uongo kinyume cha Sheria ya Makosa ya Kimtandao ya Mwaka 2015.


Katika taarifa iliyotolewa Wakili wa Serikali Daniel Masambu imeeleza kuwa mtuhumiwa huyo alikuwa anashtakiwa kwa kosa la kuchapisha taarifa za uongo katika Jukwaa la Mtandao wa Whatsapp la "Simiyu Breaking News".


Ameeleza kuwa shtaka la kwanza na la pili alitenda Desemba 03 na 04, 2021 mtuhumiwa huyo aliandika kwenye jukwaa hilo maneno ya kumkashifu Rais Samia Suluhu Hassan.


Shtaka la tatu ni kutumia namba ya simu  0764996612  isivyo kihalali iliyokuwa imesajiliwa kwa jina la Hollo Yonas bila kuwa na kibaki kutoka mamlaka husika.


"Katika makosa hayo yote mshtakiwa amehukumiwa kutumia kifungu cha miaka mitatu jela na faini ya Sh5 milioni kwa kosa la kwanza, miaka miwili jela na faini ya Sh5 milioni kwa kosa la pili na miaka miwili jela pamoja na faini ya Sh5 milioni kwa kosa la tatu," amesema Masambu.


Chanzo: Mwananchi


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright 2025 EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo