Mwanaume
mmoja raia wa Misri amefyeka mikono yake yote miwili kwa kuitega kwenye
njia ya treni iendayo kasi ili kukomesha wizi wake uliokithiri.
Ali
Afifi, mwenye umri wa miaka 28, dhahiri alikuwa akitishwa mno na mazoea
ya uhalifu wake kiasi cha kujipa hukumu kwa kuifyeka mikono yake
mwenyewe.
Mwanaume
huyo, dhahidi alikuwa akiongozwa na hukumu za Sheria ya Sharia,
ameifyeka bila huruma mikono yake yote katika adhabu yake ya kujihukumu
mwenyewe.
Uamuzi wake unaonekana
kabisa kwamba umetokana na mafundisho ya Kiislamu ya Sheria ya Sharia -
kanuni, masharti na hukumu ambazo zinataarifu kila chembe ya uhai kwa
wote walio katika Uislamu.
Afifi alisema 'maradhi'
yake ya kuiba yalianza akiwa mdogo, kwanza kwa kuchukua vyakula vya
wenzake kwenye Shule ya Msingi. Kisha ikaongezeka kwenda kwenye bishaa
katika maduka na hadi hivi karibuni alikuwa akiwakwapulia watu simu za
mikononi na vito vya dhahabu.
Alisema alikuwa akitoa fedha alizopata kutokana na wizi huo kwa watoto na familia za mafukara.
Lakini Afifi hakuwa na
uwezo wa kuendana na hatia hiyo na kuamua kukata kabisa mikono yake na
kuhitimisha kabisa mazoea yake hayo yasiyoweza kudhibitika.
Alisema anataka kusaidia
mji wake anaoishi, kuboresha majengo na kujenga kituo cha vijana. Pia
anataka kuoa lakini ana mashaka kama mwanamke wa Misri anaweza kumkubali
kwa sababu ya historia yake ya wizi.
Mfumo wa sheria wa Kiislamu
unahusika na mambo mengi yanayoelezewa katika sheria ya kidunia pia
kutaarifu maamuzi ya kila siku binafsi na mambo ya kidunia, ikiwamo
usafi, kufunga, kuswali, lishe, siasa, kujamiiana na sheria za ndoa.
Tafsiri ya sheria hiyo kwa
Waislamu inatofautiana kati ya tamaduni, lakini inakubalika katika nchi
kadhaa kwamba kurudia kuiba adhabu yake ni kukata mkono huo.
Kawaida, mtu aliyekamatwa
akiiba anaweza kushitakiwa kwenye mahakama ya Kadhi ambako wanasheria wa
Kiislamu watatoa mwongozo kuhusiana na suala hilo.
Lakini kwa Afifi,
anayetokea katikati ya mkoa wa delta ya Nile wa Tanta, Misri, aliamua
akijua hukumu itayomkabili, kwa mujibu wa 'ubashiri wa sheria' hiyo.
Kwa mujibu wa Sharia, kuiba kunachukuliwa kama moja ya makosa makubwa kama ilivyoainishwa katika Kur'an Tukufu.
Mahakama ya Kadhi inaweza
kutoa hukumu ya majeraha ya aina fulani kwenye mkono huo kwa
aliyekamatwa akiiba kwa mara ya kwanza, kama kupitisha gari taratibu juu
ya mkono huo.
Katika nchi kama Iran,
Saudi Arabia na kaskazini mwa Nigeria, adhabu ya kukatwa kiungo kwa
kurudia kuiba bado inatumika. Nchini Misri, hatahivyo, mahakama
hazijaruhusiwa kutoa hukumu ya kukata viungo kwa miaka mingi sasa.
Mwaka
jana, hatahivyo, chini ya serikali mpya ya Muslim Brotherhood, Mbunge
Adel Azzazy, kutoka chama cha Nour, alipendekeza muswada wa kukata
viungo kwa makosa fulani.
Na mdodosaji