Jeshi la polisi mkoa wa Iringa linamshikilia mtu mmoja kwa tuhuma za kujihisisha na matukio ya utapeli kwa kujivika kivuli kuwa yeye ni Afisa wa Idara ya Usalama wa Taifa makao makuu ambapo alitumia nafasi hiyo kufanya matukio mbalimbali likiwemo la kuwashawishi wajumbe wa mkutano mkuu wa Chama Cha mapinduzi CCM kumchagua mmoja ya wagombea katika nafasi ya Uenyekiti wilaya kama maagizo ya viongozi ngazi za juu.
Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa, ACP Allan Bukumbi amesema mtuhumiwa huyo amekamatwa akitekeleza uhalifu huo huku akiwa na gari ndogo aina ya Vox Wagon yenye namba za usajili T858 DVE Mali inayotajwa kutapeliwa Jijini Dar es Salaam.