Akereka na hotuba ya Rais na kuamua kuchoma mto TV yake

Mwanaume wa eneo la Kakamega huko nchini Kenya ameelekeza hasira zake kwenye televisheni yake, baada ya kutazama habari zilizomvunja moyo kwa kukosa matumaini ya kupunguzwa kwa gharama ya maisha.


Mwanamume huyo aliyetambulika kama Okoth Vicky, alikereka alitazama habari wakati Rais William Ruto alipowaomba Wakenya kumpa muda wa mwaka ili apunguze gharama ya ju ya maisha.


Okotha alipoona bei ya vyakula haitapunguzwa hivi karibuni, aliamua kuichukua TV na kuiteketeza moto nje ya nyumba yake.


"Sikudhania itafikia hatua kwamba sitakuwa na haja ya kutazama taarifa za habari. Serikali imesema bei ya unga itapungua mwaka ujao. Kwa hivyo, sitaki kuona habari tena. Sitaona sura ya Rais tena kwa TV. Wacha iishie hapo," alisema huku akichoma moto TV yake. Mwanamume huyo ambaye ni msanii, alisema Rais Ruto hajatekeleza ahadi alizowapa wananchi wakati wa kampeni, hata ingawa wengi walikuwa na matumaini makubwa naye kuwa angepunguza gharama ya maisha.


Wakati wa kampeni, Ruto alikuwa akiangazia jinsi uchumi ulivyozorota, na kupa kwamba, ataleta mabadiliko yafaayo ambayo yatakuwa mora kuliko ya Rais mstaafu Uhuru Kenyatta.

Chanzo: TUKO.co.ke


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright 2025 EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo