NAIBU MEYA ILALA AZUNGUMZIA UONDOAJI WA MABANGO YA MATANGAZO

Naibu meya wa manispaa ya Ilala Mhe Kheri Kessy, Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake hawapo pichani, kuhusu uondoaji wa mabango ya matangazo katika manispaa ya ilala ambapo ameyataja baadhi ya makampuni ambayo ni wadaiwa sugu ni Makampuni ya simu, Soda na Vinywaji vikali.Ambayo inadaiwa zaidi ya Tsh 1  bilioni na milioni 400.

Aidha amesema wadaiwa wote sugu wameshapewa notisi ya miezi 6 na kushindwa  kutii agizo hilo, hivyo kwa mujibu wa sheria za Halmashauri ya manispaa Ilala imeamua kuchua hatua ya kuyaondoa matangazo hayo. 
 
Aidha ameongeza kuwa utekelezaji huu unaendana sambamba na kuwachukulia hatua za kisheri kwa wale wate walioshindwa kulipia matangazo yao kwani yanarudisha nyuma maendelo ya halmashauri kutokana na manspaa kutegemea mapato kutoka katika matangazo hayo pamoja na vyanzo vingine katika utendaji wa shughuli zake.
Picha na Philemon Solomoni
Habari kwa hisani ya Full shangwe


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright 2025 EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo