Mgombea urais wa chama cha ADC apatikana rasmi

 Wanachama wa chama cha ADC wakishangilia mara baada ya kumtangaza mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Zanzibar katika mkutano wa kamati kuu uliofanyika leo katika Hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam.
Wanachama wa chama cha ADC wakipata urudani kutioka kwa kijana wao wa burudani katika mkutano mkuu wa chama hicho wa kumtangaza mgombea urais wajamhuri ya muungano wa Tanzania,mgombea urais wa Zanzibar na mgombea mweza katika nafasi hiyo, katika mkutano uliofanyika Hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam leo.
Katibu mkuu wa chama cha ADC, Lidia Bendela akizungumza na wajumbe wa mkutano mkuu wa chama cha ADC ambao walikuwa wanawatangaza wagombea wa Urais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania na wa Zanzibar pamoja na Mgomea mweza katika mkutano uliofanyika Hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam leo.
Mgombea wa Urais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, Chifu Lutalosa Yemba akigombea nafasi ya urais kupitia chama cha ADC akizungumza mara baada ya kutangazwa kuwania nafasi hiyo leo katika mkutano wa kamati kuu wa chama cha ADC  uliofanyika leo katika Hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa chama cha ADC na Mgombea mwenza wa urais kupitia chama cha ADC, Said Miraji Abdala akizungumza mara baada ya kutangazwa kugombea nafasi ya mgombea mweza kupitia chama hicho leo katika mkutano wa kamati kuu uliofanyika katika hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam leo.
 Mgombea wa urais wa jamhuri ya muungano watanzania kupitia chama cha ADC,Chifu Lutalosa Yemba na Mgombea wa urais wa Zanzibar,Hamad Rashid Mohamed wakipunga bendera za chama chao kuashiria ushindi wa kuwania nafasi za juu uongozi katika chama hicho, katika mkutano wa Kamati kuu uliofanyika katikahoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam leo.
Picha na Avila Kakingo,Blogu ya Jamii.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright 2025 EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo