Siku chache kabla ya agizo la mabasi ya abiria kutakiwa kuanza kuitumia stendi ya mabasi Tandala wilayani Makete mkoani Njombe, ufafanuzi wa baadhi ya mambo ikiwemo kushusha na kupakia abiria umetolewa na Halmashauri hiyo
Katika mahojiano maalum na mtandao huu ofisini
kwake, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo William Makufwe amesema pamoja
na kwamba mabasi yanatakiwa kushusha na kupakia abiria katika stendi ya
Tandala, lakini endapo kuna abiria wagonjwa waliopo kwenye basi husika
watawaruhusu kwenda kuwashusha hospitali ya Ikonda na basi hilo kurudi stendi
ya Tandala
Hiyo ni kutokana na sintofahamu iliyojitokeza
kwa baadhi ya watu baada ya tangazo la kuanza kutumika kwa stendi hiyo ya
Tandala kuanzia Oktoba 1, 2022, hivyo kituo hiki kikataka kufahamu kuhusu
baadhi ya abiria wagonjwa kushushiwa stendi ya Tandala badala ya Ikonda
hospitali, ambapo amesema hilo litaruhusiwa huku akitoa onyo kwa wanaopotosha
taarifa za matumizi ya stendi hiyo Kwa kuwa upo uwekezaji uliofanyika katika
eneo hilo hivyo inatakiwa kuanza kutumika
Amesema kuanza kutumika kwa stendi ya mabasi Tandala ni utekelezaji wa agizo la muda mrefu wa vikao vya madiwani wa Halmashauri hiyo ikiwemo Kamati ya Fedha ambapo walikubaliana kuifufua stendi hiyo ili ianze kutumika.
Bofya hapo chini kuona video hiyo