Mkuu wa mkoa wa Njombe Antony Mtaka amesema kwa sasa wao kama viongozi wanaangalia maendeleo ya wananchi na si vinginevyo huku akiwaonya madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Makete wanaopenda malumbano kuendelea nayo na hata wakihitaji vyeti vya malumbano yeye yupo tayari kuwapa
Amesema mwaka 2025 madiwani hao watafika kwenye ofisi za Chama cha Mapinduzi kuchukua fomu za kugombea udiwani na si Uenyekiti wa Halmashauri hivyo kumtaka Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Makete William Makufwe kuendelea kuchapa kazi kwa manufaa ya wilaya hiyo