Serikali yaongeza Idadi ya wanafunzi watakaopatiwa Mikopo

Idadi ya wanafunzi  watakaonufaika na mikopo kutoka Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu- HESLB imeongezeka kutoka 33,000 hadi 40,000 kwa mwaka wa masomo wa 2018/19.
Akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Abdulrazaq Badru amesema bodi hiyo imeongeza idadi ya zaidi ya wanafunzi 7,000 ukilinganisha na 33,000 waliopata mwaka jana.
Badru amesema zimetengwa jumla ya Sh. 437 bilioni kwa ajili ya kutoa mikopo hiyo, ambapo pia HESLB imeongeza wigo wa kutoa mikopo kwa wanafunzi wa stashahada.
Amesema hapo awali mikopo ilikuwa inatolewa kwa wanafunzi wa ngazi ya stashahada wa kozi za ualimu, na kwamba kwa sasa maeneo yenye uhitaji wa wataalamu yatapewa fursa.
Katika hatua nyingine, Badru amesema bodi hiyo imefungua dirisha la kupokea maombi ya mikopo.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo