CHADEMA Wapandisha Bendera "zilizoshushwa" na Makamu wa Rais

Mwenyekiti wa Wazee Taifa (CHADEMA) na Mjumbe wa Kamati kuu, Mheshimiwa Hashimu Juma Issa, amefungua matawi mapya matatu(3) na kupandisha bendera mpya katika matawi matano(5) Katika majimbo ya Mahonda, Donge na jimbo la Bwimbwini yaliyopo mkoa wa Kaskazini Unguja, kanda ya Unguja.
Mhe. Hashimu Juma Issa amefungua matawi hayo akiwa katika ziara yake ya hamasa na uimarishaji wa chama katika mkoa huo wa Kaskazini Unguja ya siku mbili iliyoanza hapo jana Aprili 09,2018, katika Wilaya ya Kaskazini A.
Akiwa ameongozana na viongozi wa kanda ya Unguja, Mkoa wa Kaskazini Unguja na maofisa kutoka ofisi ya Makao Makuu Zanzibar, amerudisha bendera iliyoshushwa wakati wa ziara ya Makamu wa Rais, aliyoifanya hivi karibuni katika kisiwa cha Unguja na Kuwapatia kadi wanachama wapya zaidi ya 45 waliojiunga na chama.
Kabla ya Uzinduzi na Ufunguzi wa matawi hayo, Mheshimiwa Hashimu Juma Issa alikutana na Baraza La Uongozi la wilaya ya Kaskazini A na mabaraza ya Uongozi ya majimbo ya Mahonda, Bwimbini na Donge na kupokea taarifa za hali ya chama pamoja na utendaji wa viongozi hao.
Katika hotuba yake kwa viongozi wa wilaya na majimbo hayo, Hashimu Issa aliwahakikishia viongozi hao wa chama, ngazi ya wilaya na majimbo juu ya uimara wa chama na kuwataka kufanya kazi kwa juhudi, umoja, upendo na mshikamano.




Aidha, Kabla ya ufunguzi wa matawi hayo, Mheshimiwa Hashimu alikagua misingi iliyopo katika matawi hayo na kuwataka viongozi wa maeneo hayo kuamka na kuongeza kasi ya mapambano kwa kuimarisha chama kwani ukombozi wa demokrasia na haki upo karibu.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo