Inadaiwa kuwa mtuhumiwa alikataa wito wa mumewe was kumtaka kurudia kupika chakula baada ya kutokushiba, hivyo akashikwa na hasira na kumchoma kisu.
Mauaji hayo yalitokana na ugomvi baina ya mtuhumiwa ambaye inadaiwa kuwa alikataa wito wa mumewe kupika chakula baada ya kutokushiba.
Akizungumzia kuhusiana na tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Lucas Mkondya, amesema tukio hilo lilitokea juzi mkoani humo.
Kwa mujibu wa Mkondya, mwanamume huyo alikufa papo hapo baada ya kuchomwa kisu na mke wake.
Alisema siku ya tukio majira ya saa 1:30 usiku, mwanamke huyo alimwandalia mume wake chakula na kumpatia.
“Kile chakula kilikuwa kidogo, mume wake, Ahmed Salim, alimtaka arudi jikoni kwa ajili ya kupika tena chakula kwa kuwa hakikumtosha.
Hapo ndipo palitokea ugomvi wakalumbana na wakaendelea kugombana na mkewe akachukua kisu na kumchoma kifuani na kufa papo hapo,” alisema Kamanda Mkondya.
