Afisa Habari wa Jeshi hilo, Mrakibu Msaidizi wa Magereza, Lucas Mboje ameeleza kuwa katika maadhimisho hayo, Rais alitoa msamaha kwa wafungwa ambapo baadhi walitoka siku hiyo hiyo na wengine walibaki kumalizia muda wao, kutokana na kupunguziwa adhabu.
“Jumla ya wafungwa 585 kati ya 3,319 waliopewa msamaha waliachiliwa Aprili 26, mwaka huu. Wafungwa 2,734 akiwemo Sugu na Masonga walibakia gerezani kumalizia sehemu ya kifungo kilichobaki baada ya msamaha wa Rais Dkt John Pombe Magufuli”, amesema Mboje.
Wawili hao walikuwa katika Gereza la Ruanda Jijini Mbeya walikokuwa wakitumikia kifungo cha miezi (5) baada ya kukutwa na hatia ya kutoa lugha ya kumkashifu Rais Dkt. Magufuli ambapo hukumu yao ilitolewa Februari 26, 2018 na Hakimu Mkazi Mfawidhi, Michael Mteite baada ya na ushahidi wa upande wa mashtaka.
Mh Joseph Mbilinyi (SUGU) ameachiliwa huru leo Mei 10, na baada ya kuachiliwa kwake Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Freeman Mbowe amesema bado watakata rufaa kuhusu kesi hiyo.
