"Hii ni dharau kubwa" -Rais Magufuli

Rais John Magufuli ametoa mwezi mmoja kwa taasisi za Serikali na watu binafsi wanaodaiwa Sh 41.4 billioni na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kuhakikisha wanalipa fedha hizo  ili ziweze kutumika kujenga viwanda vingine na kwamba kutolilipa jeshi ni dharau kubwa

Rais ametoa maagizo hayo leo, alipokuwa akizindua kituo cha uwekezaji cha Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), jijini Dar es Salaam baada ya Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (CDF), Venance Mabeyo kumuomba kusaidia kulipwa kwa madeni hayo.
Mabeyo amemueleza Rais kuwa katika changamoto waliyonayo ni pamoja kutolipwa madeni na watu wanaofanya nao kazi na kwamba kupitia Suma JKT walitengeneza na kukopesha watu mbalimbali matrekta yenye thamani ya Sh 40 bilioni na zilizolipwa ni Sh 2 bilioni na kubaki deni la Sh 38bilioni.
Aidha ameongeza pia Suma JKT wanaolinda taasisi za Serikali wanadai Sh 3.4 billion, hivyo kufanya madeni hayo kwa Sh 41.4 billioni.
"Tunaomba utusaidie kutia msukumo katika hili kwa sababu taasisi za Serikali zina lugha ya tutalipa tu endeleeni na ulinzi tu" amesema Mabeyo.
"Waziri wa Ulinzi, Katibu mkuu wa wizara ya Ulinzi waandikieni barua na mnitumie nakala ili niwe nafuatilia watakapokuwa wameanza kulipa. Nataka fedha hizo zipatikane ili ziweze kutumika kujenga viwanda vingine. Rais Magufuli.
Ameongeza "Mtu anaanzaje kuacha kulipa fedha ya jeshi, hii ni dharau kubwa, raia wadharauliwe na Jeshi pia?”


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo