Heche: Bora wakoloni Kuliko CCM

Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche amemtaka Waziri wa Maji, Dk. Isaack Kamwelwe kuweka wazi mahali zilipo dola milioni 500 kutoka Serikali ya India ambazo waliahidi zipo kwa ajili ya miradi ya maji kijijini

Mh. Heche ameyasema hayo leo Bungeni katika mjadala wa bajeti ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji ya mwaka 2018/19, ambapo Mbunge huyo ameshangazwa kuona mpaka hata kijijini kwa Mwalimu Nyerere hakuna maji.
Mh. Waziri ulituambia kuna dola milioni 500 za serikali ya India kwa ajili ya maji vijijini utueleze ziko wapi. Kama mmesahau sisi wengine tuna kumbukumbu. Yaani hata kwa Mwalimu Nyerere hakuna maji? Nimezaliwa Tarime kuna maji, lakini kadri tunavyozidi kwenda mbele tunarudi nyuma, ndiyo maana tunasema bora wakoloni kuliko serikali ya CCM.
Heche ameongeza  "Hata mabomba ya wakoloni waliyoyaacha yameharibika".
Pamoja na hayo Mbunge huyo amesema hata suala la kuundwa tume kutokana na miradi ya maji kukwama limewahi kujadiliwa mara nyingi lakini ni kama linapigwa danadana.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo