Kessy amesema hayo Bungeni leo Mei 09, 2018 wakati wa kuchangia mjadala wa kupitisha makadirio ya mapato ya matumizi ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji na kusema kuwa Wizara ya Maji inaongoza kwa kutumia vibaya kodi za wananchi.
“Haiwezekani mheshimiwa Rais anajitahidi kutoa pesa lakini idara ya maji ni kama mfereji unatoa tu watu, ndugu zangu tuwe na uchungu na nchi hatuwezi kukubali kuibiwa namna hii, maji ni uhai Namanyele tunapata maji asilimia 16, nilizungumza hapa mimi Mbunge ninakaa siku tatu siogi” amesema Kessy.
Kessy pia aliongeza kuwa miradi migi ya maji katika mkoa wa Rukwa imekumbwa na ufisadi na baadhi inamilikiwa na viongozi wa serikali na walimtaka kutoongeea suala hilo Bungeni.
Pamoja na hayo, Kessy ameongezea kwa kusema “viongozi wakubwa ndiyo wenye miradi hii wanajulikana, kwa ushahidi walinitafuta nizungumze nao na mimi niliwakatalia eti mbunge nyamaza ili waibe zaidi, haiwezekani” .
Baadhi ya miradi ya maji yenye matatizo kwa mujibu wa Mbunge huyo ni Kamwanda uliogharimu milioni 200, Matala (450 milioni) Bwawa la Mfili (Bilioni 1), Isile (bilioni 1.1), mradi wa kwenda Isale (5.4 bilioni)
