Sugu na Masonga Hawastahili Pongezi - Zitto

Mbunge wa Kigoma Mjini,  Zitto Kabwe amegoma kumpa pole Mbunge wa Mbeya Mjini , Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ pamoja na mwenzie Emmanuel Masonga baada ya kutoka gerezani kwa madai kuwa  viongozi wote wa upinzani kwa sasa ni wafungwa watarajiwa.
Zitto Kabwe ameandika katika ukurasa wake wa mtandao wa Twitter kwamba amefurahi kuona wako huru huku akiamini kuwa  kukaa kwao gerezani kumewaongezea ari ya kupigania Demokrasia nchini.
“Nafurahi kuwa Mbunge Mbeya Mjini Ndg. Joseph Mbilinyi (Sugu) na mdogo wangu Emmanuel Masonga wametoka Gerezani! siwapi pole, maana katika nyakati za Udikteta wapinzani wote ni wafungwa watarajiwa. Naamini kukaa kwao gerezani kumewaongezea zaidi ari ya kupambania Demokrasia pana ya Nchi yetu.Watawala mjue sasa kuwa vifungo vya Uonevu, kututishia Maisha na hata kutupiga risasi havita turudisha nyuma kwenye kupigania demokrasi ya nchi yetu.“ameandika Zitto Kabwe.
Sugu ameachiwa huru leo Mei 10, 2018 kutoka gereza la Ruanda, Mbeya alipokuwa akitumikia kifungo cha miezi mitano kwa makosa ya uchochezi.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo