Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Rukwa, Aida Joseph Kenan amehoji bungeni mjini Dodoma kuhusu ununuzi wa ndege mpya ya Bombadier Q400 aliyoipokea Mhe. Rais Magufuli hivi karibuni, iwapo ndicho kipaumbele cha taifa la Tanzania
Mhe. Aida amesema kwamba ingekuwa vyema kama serikali ingenunua meli na kuzitawanya sehemu mbalimbali nchini kwani wananchi wengi wa hali ya chini waliopo vijijini wanatumia meli katika kusafirisha mazao na shughuli zao zingine na hawana uwezo wa kupanda ndege.
Aidha, amewataka mawaziri kumshauri Rais na Bunge kuisimamia serikali kwa ajili ya manufaa ya Watanzania wote.