Wasichana 17,840 Iringa kuchanjwa

Wasichana zaidi ya 17,840, Mkoani Iringa wanatarajiwa kupata chanjo ya Saratani ya Mlango wa Uzazi ifikapo mwishoni mwa mwezi April mwaka huu

Mratibu wa Afya Mkoani humo, Naftali Mwalongo, amebainisha hayo wakati wa kikao cha uzinduzi wa kamati ya uhamasishaji Mkoani Iringa kuwa chanjo ya HPV itatolewa kwa awamu ikiwa na lengo la kutoa kinga kwa watoto wa kike wenye umri kati ya miaka 9 hadi14.
Kwa upande wake, Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Iringa, Lukas Kambelenje, amesema ni mara ya Kwanza chanjo ya HPV kufanyika Mkoani humo, 
Aidha ameitaka  Kamati hiyo kutoa ushirikiano wa kutosha katika kuhamasisha wazazi kuwapeleka watoto wao kupata Chanjo hiyo


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo