BAADHI ya wananchi wa kijiji cha Tandala wilayani Makete mkoani Njombe wameibua tena hoja ya kutaka kunywa pombe wakati wa asubuhi siku za mapumziko huku baadhi yao wakiunga mkono serikali ya kijiji kufuata utaratibu uliopo.
Hoja hiyo imeibuka jana Machi 22, katika mkutano wa kijiji cha Tandala
Mkutano huo umeongozwa na viongozi wa serikali ya kijiji ambapo baaadhi ya wananchi waliuomba uongozi wa serikali ya kijiji kuwacha wafanyabiashara wafungue mapema vilabu vya pombe siku za juma mosi na juma pili kwa sababu ni siku za mapumziko
Wamewasisitiza wananchi wa kata ya Tandala kuendelea kufuata kanuni na sheria za nchi huku wakisema siku za jumamosi na jumapili vilabu vya pombe vyote vifunguliwe kuanzia saa sita mchana kama serikali inavyotaka.
Wananchi wengine wa Tandala wemeunga mkono kauli hiyo ya viongozi wao huku wakisema kwa watumiaji wa pombe wafuate sheria za nchi kwani serikali haina mchezo na hilo.
Pia wamesema hakuna kiongozi yoyote anaeweza kuwaambia wananchi wafanye jambo ambalo ni kinyume na sheria.
Hivi karibuni waandishi wetu walishudia mkuu wa kituo cha polisi Tandala akiwakamata wanaofungua vilabu vya pombe wakati wa asubuhi.
Katika mkutano huo mbali na hoja hiyo zimezungumzwa ajenda mbali mbali za maendeleo ya kijiji, ikiwemo kusoma mapato na matumizi ambapo wananchi waliipokea taarifa hiyo.
Bonyeza Play hapo Chini uipate kiundani:-
Bonyeza Play hapo Chini uipate kiundani:-
