"Sitishwi wala sitishiki" - Rais Magufuli

Rais Dkt. Pombe Magufuli amesema uwepo wake madarakani ni kutaka kuwatoa watanzania katika shida mbalimbali walizokuwa nazo na kuwapelekea eneo ambalo watakula raha ili siku atakapokuja kufa basi hata Mungu ampe nafasi ya kuwaongoza Malaika mbinguni

Dkt. Magufuli ametoa kauli hiyo wakati alipokuwa anazungumza na wananchi wa mkoa wa Singida muda mchache kabla ya kukizindua kiwanda cha mafuta ya Alizeti Mount Meru Millers kilichojengwa mkoani humo.
"Nataka niwahakikishie watanzania kuwa mna Rais kweli kweli, jiwe kweli kweli. Sitishwi wala sitishiki mimi jukumu langu ni kwaajili ya watanzania, nikuhakikisha nawavusha watanzania kutoka mahali kwenye shida na kwenda mahali kwenye raha. Ninajua hiyo ndio itakuwa sadaka yangu kwa watanzania ili kusudi hata siku moja nikienda huko mbinguni Mungu atakaponihitaji, akanichague kutokana na mimi nilikuwa kiongozi mzuri hivyo unaweza hata kuongoza Malaika polepole kwasababu ninajua kuna maisha baada ya maisha ya hapa duniani", amesema Dkt. Magufuli.
Pamoja na hayo, Dkt. Magufuli ameendelea kwa kusema "ndio maana nawaomba sana viongozi wa dini, masheikh na wale watu mbalimbali katika imani zao tuitangulize Tanzania kwanza, tusitumike".
Kwa upande mwingine, Rais Dkt. Maguli amewataka wananchi kufanya kazi kwa bidii ili waweze kujikomboa na kujiongezea kipato cha maisha.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo