Rais Magufuli akiri kupata tabu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli amekiri kupata wakati mgumu katika uteuzi wa Baraza la Mawaziri kutokana na kuwa Mkoa wa Singida kujaa Wabunge wenye sifa zote za kushika nyadhifa hizo

Akiwa katika uzinduzi wa kiwanda cha mafuta ya alizeti mkoani  Singida, Rais Magufuli amesema kwamba anafurahishwa sana na utendaji kazi wa wabunge hao kiasi kwamba alitamani kuwateua wote kuwa katika baraza lake.
Rais amesema kwamba Wabunge wa mkoa huo wamekuwa wakimfurahisha katika utendaji kazi wao wa kuwatumikia wananchi.
"Msema kweli ni mpenzi wa Mungu. Wabunge wa Singida hawajaniangusha.  Nilikua napata shida katika kuteua Mawaziri katika mkoa huu, kila unayemona ana sifa kila unayemuona anasifa ningejikuta nateua wote badala ya mikoa mingine" Mh. Rais. 
Ameongeza "Sasa unajiuliza watatoka wote Singida? lakini kwa kwa inatakiwa ku-balance ndio hivyo,  lakini Singida 'You have all the qualification, everybody'. Nawaambia ukweli kila mmoja mimi CV yake ninayo. Hamjaniangusha mnafanya kazi. Fanyeni kazi kwa manufaa ya watu. Nawapenda,".
Aidha Rais Magufuli amekiri kufurahishwa na wakazi wa Singida kwani wamekuwa wakitekeleza kauli ya 'Hapa Kazi Tu' kwa vitendo kwa  kulima sehemu kubwa ya mkoa huo ambapo amejionea mwenyewe akiwa katika safari ya gari kuelekea mkoani hapo.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo