Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Avemaria Semakafu amefunguka na kuweka wazi utata ulioibuka kuhusu kigezo cha umri wa kujiunga na masomo ya kidato cha tano na sita na kusema taarifa ambayo inasambaa imekuwa na makosa"Kumetokea makosa ya kiandishi, miaka ni 25 ya kujiunga sekondari na sio 20 kama ambavyo inasomeka kwenye ile karatasi" alisema Semakafu