Ole Sosopi amesema hayo leo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari na kusema kuwa Katibu Mkuu wa BAVICHA yeye ataongoza viongozi wa Baraza hilo la vijana Mbeya kwenda kuwaona Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi na mwenzake Katibu wa CHADEMA Kanda ya nyanda za juu kusini, Emmanuel Masonga ambao wamefungwa katika gereza la Rwanda Mbeya.
"Mimi kama Mwenyekiti nitaongoza msafara wa viongozi wa BAVICHA katika level zote kwa mkoa wa Dar es Salaam kuelekea gereza la Segerea kesho kuwatembelea viongozi wetu lakini pia Katibu Mkuu na Muhamasishaji Vijana Taifa wao wataelekea Mbeya kwa ajili ya kumtembelea kamanda Sugu na Masonga katika kipindi hiki cha mapumziko tutafanya shughuli zetu kwa kuwatembelea makamanda wetu na kuwatia moyo na kuwaeleza kwamba mapambano huku nje yanaendelea japo wao wapo magerezani" alisema Sosopi
Viongozi sita wa CHADEMA akiwepo Mwenyekiti wa chama hicho, Katibu Mkuu Dkt. Mashinji, Mbunge Msigwa, Mbunge John Mnyika, Mbunge Ester Matiko na Salum Mwalimu wapo mahabusu licha ya Mahakama kuwapatia dhamana toka Alhamisi hata hivyo watasalia rumande hadi kesi yao itakapotajwa tena wiki ijayo tarehe 3 Aprili ambapo wataletwa mahakamani kukamilisha masharti ya dhamana.
